Mwandishi wa habari mkongwe afariki dunia

Mwandishi wa habari za siasa na jamii wa siku nyingi Casmiry William Kayumba alifaliki kutokana na kifo cha ghafula ambacho mpaka dakika hii haijaeleweka chanzo cha mauti hiyo iriyo musibu akiwa nyumbani kwake eneo la Ndera.

Mwandishi wa habari afariki dunia

Kutokana habari turizo pata kutoka kwa jamaa wa marehemu, ni kwamba Casmiry aliamuka mzima siku ya jumanne, akashinda nyumbani kwake na ilipo fika majila ya jioni alijisikia kuumwa tumbo na mkewe akamwita jirani aliyempeleka Hospitali ya Ndera na hapo hospitali arizidiwa ikabidi ahamishiwe Hospitali kuu ya wilaya ya Gasabo, Kibagabaga na kwa bahati mbaye marehemu Casmiry akaaga dunia akiwa njiani akafikishwa hospitalini akiwa tayari ameisha kata roho.

Casmiry William Kayumba alizariwa miaka 59 iliyo pita  nchini Rwanda, na maisha ya utotoni alianzia Karagwe nchini Tanzania amabako wazazi wake waliishi kama wakimbizi wa siasa waliokimbia mauaji ya ki  kabila yaliyotokea nchini Rwanda miaka ya 1959 -196.

 Masomo ya shule ya msingi alianzia Kayisho primary school 1971 -1978, sekondali alisomea shule ya sekondari ya Bukoba (o’level) na kumalizia elimu ya sekondali Muzumbe High School 1985.

Kuanzia mwaka 1987 -1991 alijiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam (Dar Universty) ambako alihitimu shahada ya Ualimu.

Baada ya kuhitimu masomo yake, munamo mwaka wa 1991, Marehemu Casmiry aliajiliwa na gazeti moja la ki binafsi lililokuwa likitoka kila siku kwa lugha ya kingereza lijulikalo kama Business Times akiwa mwandishi wa habari za siasa na itakumbuka marehemu alitowa mchango mkubwa wakati vita ya kuyikomboa Rwanda iliyokuwa imeanzishwa na majeshi ya RPF- Inkotanyi wakati huo akiwa elimisha wasomaji ni kwa nini majeshi hayo yamevamia nchi ya Rwanda.

Mwaka 1992 alibahatika kupata nafasi ya kwenda kupata mafunzo ya uandishi wa habari amabako alichukuwa kozi ya mwaka mmoja nchini Marekani.

Munamo mwaka wa 1992 Casmiry alipatwa na ajali mbaya ambako pikipiki ya kazi aliyo kuwa akitumia iligongwa na gali ajali hiyo ilimpeleka Hospitari kuu ya Dar es Salaam Muhimbiri ambako alilazwa kwa mda wa miaka miwili.

Baada ya kutoka hospitalini hapo, aliendeleya na matibabu katika Hospitali ya CHK wakati huo nchi ya Rwanda ilikuwa tayari imekombolewa yeye kama wanyarwanda wenzake alikuja nyumbani Rwanda.

Munamo mwaka wa 1996, marehemu Casmiry alianzisha magazeti mawili yake binafsi RWANDA NEWS LINE  na UKURI lakini alifahamika zaidi kwenye gazeti la UKURI likiwa na maana ya “ukweli” likiwa ni miongoni mwa na magazeti makongwe nchini Rwanda ambako atakumbuka kwa makara zake za uchambuzi na kuandika habari za ukweli ambazo zilipendwa na wengi.

Mpaka mauti yanamufika, Casimiry alikuwa mwandishi wa habari wa gazeti la RUSHYASHYA akiwa kama mhariri wake mkuu . Marehemu Casmiry W.Kayumba, ameacha mke na watoto 4. Atazidi kukumbukwa kwa ucheshi, upole, mtu asiyependa makuu na mpatanishi wa watu na mwandishi wa habari mwenye kipaji.

Gakwandi James

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *