Clabu ya APR FC isitafutie mchawi mbali na timu.

Clabu ya APR FC ambawo ndiwo mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu nchini Rwanda kwa musimu uriwo pita 2016/2017 hivi sasa imekuwa ni gumuzo aidha zuri kwa mahasimu wawo wakuu Rayon Sport huku wapenzi wa timu hiyo wakijiuriza ni tatizo gani riro yisibu timu yayo musimu huu.aprp

                                Timu ya kwanza ya APR Fc ikiwa Mulindi Byumba hapa irikuwa 1993 ni timu ya jeshi bila raia

Timu hii ambayo inamilikiwa na jeshi ra urinzi la Rwanda ikiwa ni ya pili kwa washabiki wengi, nyuma ya Rayon Sport ambayo ndiyo inayoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi kutokana na kuwa clabu kongwe, kama vile Amagaju, Kiyovu na Mukura imefikia wakati mugumu ambawo clabu hiyo ilikuwa haijawahi kuwa nao kwa muda wa miaka 23 iriyopita tangu isajiriwe na kushiriki ligi kuu.

APR FC ilianzishwa miaka ya 1993 huko Mulindi ambako ndiko kurikuwa makao makuu ya chama na jeshi, na mchezo wake wa kwanza waricheza na timu ya chama cha PSD na wachezaji wote wakati huo walikuwa wanajeshi na hapa tunawakumbuka waasisi wa timu hiyo,Viongozi warikuwa Major Musemakweri Jacques, na kocha Ruta wachezaji walikua aliyekuwa mulinda mulango (Goolkeper), Theogen, Sgt Ntagwabira JMV kwa wakati huo ambapo sasa hivi ni marehemu, Sgt Nsengiyumva Pompidu, Sgt Byusa Wilson Alias Rudifu, CPL Ndayisenga JMV, Sgt Kunde, Marehemu Ngenzi, Michel, John Gisoko, Cammarade, Kirirkiri, Eric Muhoza, Charles, Marius, na Marehemu Kabanda.apr fc

                                   Timu ya APR  FC ikiwa na wachezaji wa raia    

Ni katika harakati za ukombozi wa nchi ya Rwanda kutoka kwa mikono ya serikali ya kibaguzi ya Habyarimana ambaye yeye na jeshi lake warishindwa katika vita hiyo na jeshi la RPF – INKOTANYI rikawakombowa wanyarwanda na kutwaa nchi mwaka 1994 baada ya mauaji ya kimbari.umutoza23Marehemu Cpt JMV Ntagwabira arikuwa muchezaji mwanzirishi na kocha

 

APR FC ni clabu inayo fahamika kwa nidhamu ya hali ya juu kama ririvyo jeshi, nidhamu jeshi lililo nalo na timu vivo hivo ndivo ilivyo. Ni timu tajiri ukiringanisha na timu zingine nchini Rwanda, wachezaji wanalipwa mishahara mizuri, makocha wazuri wa kimataifa na kitaifa, na walikuwa wakinunuwa mchezaji yeyote yule wa kulipwa kutoka nje ya nchi na ndani, hapa tunawakumbuka akina Kaseruka, Ntaganda na akina Mbuyu.jimmy Mur

                                                                            Timu ya APR 2004

Kutokana na huo ubora wa wachezaji wenye viwango, hata timu ya taifa karibu robo tatu ya wachezaji wake hutoka katika clabu hiyo. Mbari na hayo uongozi wa clabu hiyo uliamua kuwatumia wachezaji wazalendo ili kuinuwa viwango vya vijana wa kinyarwanda kusudi mwishowe nao waweze kufikia kucheza soka la kuripwa (Profesional).

Hayo na mengine ndiyo yanayifanya clabu hiyo marufu kama "Igikona" (Kunguru) kama watani wao wawaitavyo, kutokana na rangi ya jezi yawo yaani nyeusi na nyeupe kuweza kuchukuwa mataji ya ubingwa wa ligi kuu mara 13 na mara 6 kombe rijurikanalo kama "Amahoro Cup"intare

                                                                                               Nembo ya APR

Kwa kipindi chote hicho cha miaka 22 iriyopita, APR FC lilikuwa ni jina kubwa tena la kuogopesha karibu clabu zote, ukiondoa Rayon Sport ambao kidogo kutokana na uwingi wa mashabiki wakati mwingine ilikuwa ikiyimudu. Timu ambayo irikuwa ikikutana APR FC, iwe nyumbani (Jijini Kigali) au iwe imeenda mikoani kirichotegemewa ni ushindi kwa APR FC.

Na japo kwa bahati mbaya timu pinzani imetokea ikafunga goli mapema, uwezekano wa kusababisha urikuwepo na ushindi vile vile. Hata kama ni Rayon Sport ambao ndio wapinzani wa jadi walilifahamu hilo kuwa APR FC ukitangulia kuyifunga bao itasawazisha na ikikufunga bao huwezi kusawazisha.

Ni musimu huu wa mwaka 2016/2017 wa ligi kuu nchini, ambapo mambo hayakuwa mazuri kwa club ya APR ambapo matokeo ya machi inazo cheza hayaridhishi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo ya jeshi la wananchi kwani ni kinyuma na kawurimbiu yao isemayo "dhamira yetu ni ushindi".

Hii timu ambayo imebadirisha makocha 3 kwenye kipindi cha mwaka mmoja, kiwango cha wachezaji ndio kinazidi kuwa chini ukiringanisha na miaka ya nyuma ambako kama turivyo taja hapo mwanzo kufungwa ilikuwa mwiko sasa timu zote zinachukuwa pointi moja au kuiyifunga.

Kwa mfano katika mechi 8 zirizo fuata baada ya kuwafunga wapinzani wao yaani Rayon Sport goli moja kwa bira, timu hiyo mechi irizo cheza mpaka tunaandika makara hii, imefunga moja (Mukura) na kufungwa moja na timu kibonde ya Gicumbi ambayo ipo juu kidogo ya mustari mwekundu wa kushuka daraja na michezo yote 6 ilitoka sale tena kwa timu ndogo za mikoani.

Tatizo kwa clabu hii kongwe ki mupira na yenye heshima, isiyo na tatizo la uchumi linatoka wapi? je mashabiki wanasemaje? zipo sababu zinazo tolewa na hawa wakereketwa tuliozungumza nawo, baadhi ya sababu ni za msingi na nyingine hazikubaliki ki musingi. Kwa mufano nianze na sababu moja wanayosema baadhi ya mashabiki inayosababisha timu yawo kukosa mabao ambayo mimi nayichukulia kama siyo sababu wanapodai timu irudisha wachezaji wa kulipwa kutoka nje ya nchi kama ilivyokuwa awali.

Hii sababu haikubaliki kwa sababu zifuatazo; kwanza tangu clabu hii ianzishe mtindo wa kuchezesha wazalendo miaka karibu mitatu iliyo pita, imechukuwa ubingwa mara mbiri na kombe la musimu uliopita wao ndio wanalo huu ni ushahidi tosha kuwa kutochezesha wachezaji wa kulipwa siyo sababu ya kukosa ushindi.

Hoja nyingine iliyotolewa na mashabiki, wanadai kiwango cha kocha Jimmy Mulisa kiko chini ukiringanisha na kiwango cha wachezaji, hivo ameshindwa kuwamudu ki mafunzo, kiufundi na kimbinu, hii hoja kidogo inaweza ikasikika, lakini siyo sababu kwani hata Zenedine Zidane alianza hivo hivo kwenye clabu ya Real Madrid na mwishowe akafaulu.

Hoja nyingine ambayo inaweza ikawa kweri, ni ile inayosema kwamba kuna kutoelewana kwenye benshi la ufundi kati ya kocha mkuu ambaye ni Jimmy Mulisa na kocha musaidizi Yves Rwasamanzi. Wanaoleta hoja hii wanatowa sababu ambayo inaonekana kuwa ya maana zaidi pale wanaposema kuwa uongozi wa timu ulifanya makosa kumunyang'anya nafasi ya kocha mkuu Yves na nafasi yake ikapewa Mulisa yeye akawa musaidizi au mushauli wake.itsi

                                    Mojawapo ya vikombe timu hiyo irivyo chukuwa wakiwa kamanda mkuu wa jeshi Gen.Nyamvumba

Wanaoleta hii hoja huenda mbali na kutowa mfano wa mwanume kumuacha mke kutokana na udhaifu wake, halafu ukaleta mwingine na yule uliye muacha kwa sababu ya udhaifu ukamwambia amusaidie mke mwenza je ukweri atamushauri na kumusaidia au atatamani naye aibike na achwe kama yeye arivyo achwa?.

Nikihitimisha makara yangu, nikizangatia sababu zote zirizo tolewa ili kutafuta ufumbuzi wa kwanini club ya APR FC imeshuka ki kiwango nawashauri wapenzi wa timu hiyo na viongozi wake wa kutotafutia mchawi mbali anayeloga timu yawe kwani mchawi yumo ndani ya benchi la ufundi na hivo ndivo nionavyo mimi.

Gakwandi James

ÒÇÇ

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *